Misaada kwa ajili ya waathirika wa kuporomoka kwa jengo Kariakoo itolewe kwenye akaunti moja-Dkt.Yonazi

DAR-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amesema msaada wa kifedha kwa ajili ya kusaidia walioathirika na kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam unatolewa kwa akaunti maalum ya maafa ya 9921159801 ambayo ipo Benki Kuu ya Tanzania na kushughulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Dkt.Yonazi ameyasema hayo leo Novemba 18, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali inayoendelea katika zoezi la uokoaji.

Amesema, akaunti hiyo ni pekee nchini ambayo inakusanya misaada ya kifedha kwa ajili ya maafa.
"Kuna watu wana nia njema kabisa ya kuwasaidia Watanzania, lakini naomba tujizuie kabisa kukusanya michango ya kifedha kutoka kwa mtu yeyote bila kupitia akaunti hii,"amesema Dkt.Yonazi.

Aidha,amesema akaunti hiyo ni maalumu imethibitishwa na serikali ili kuweza kuhakikisha misaada inawafikia walengwa na inatimiza malengo ya kutoa misaada hiyo.
Amesema kwa sasa operesheni inaendelea mpaka pale watakapokamilisha zoezi la kuokoa baadhi ya watu ambao bado hawajaokolewa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news