DAR-Serikali imesema,wamiliki wa jengo la ghorofa lililoporomoka katika Mtaa wa Mchikichini na Manyema Kata ya Kariakoo jijini Dar es Salaam wanajulikana.
Hayo yamesemwa leo Novemba 26,2024 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba wakati akizungumza katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Makoba amesema,wamiliki wa jengo hilo tayari wanajulikana na mmoja wao ameshakamatwa ambapo amewataka wananchi wawe na amani na waiachie Serikali ifanye kazi yake bila kuvuruga uchunguzi.
Vilevile Msemaji Mkuu wa Serikali ameahidi kuwa, uchunguzi wa ajali hiyo ukikamilika taarifa itatolewa rasmi kwa umma.
“Mwenye jengo hili hawezi kukosa kujulikana, tunamjua na mmoja wao ameshatiwa nguvuni kwa kwa sababu ni suala la kiuchunguzi Polisi wakiwa tayari watatoa taarifa ili tusiharibu uchunguzi.
"Niwahakikishie tu Watanzania Serikali haiwezi kushindwa,kwa hiyo tuwe na amani na majibu yatapatikana.
“Tume iliyoundwa, kamati ya uchunguzi imeshaanza kazi, hata kabla hamjaja hapa wengine walikuwa wanachukua sampuli ya baadhi ya vitu vilivyotumika katika ujenzi na wenyewe wakiwa tayari watatuambia tusiharibu uchunguzi,amesisitiza Makoba.