DODOMA-Imeelezwa kuwa, miradi ya ufungaji wa mifumo ya umeme jua ipatayo 20,000 ipo mbioni kuanza katika maeneo ya visiwani na makazi yaliyo vijijini ambayo hayajafikiwa na Gridi ya Taifa.

"Mradi huu unahusisha kufunga na kusambaza mifumo itakayozalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua katika makazi yaliyo vijijini ambayo hayajafikiwa na Gridi ya Taifa hasa visiwani kwa kufunga mifumo ipatayo 20,000 ndani ya miaka mitatu, "alisema Mhandisi Saidy.