MTENDAJI WA KIJIJI JELA MIAKA 20 KWA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI WILAYANI SONGWE

SONGWE-Mahakama ya Wilaya ya Songwe mkoani Songwe imemhukumu,Bw.Assan Jacob Kalinga aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Mbuyuni katika halmashauri hiyo adhabu ya kwenda jela miaka 20.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kosa la ufujaji na ubadhirifu Kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura 329 Mapitio ya Mwaka 2022,

Ikisomwa pamoja na Aya ya 21 ya Jedwali la kwanza na Kifungu cha 57(1) na 60(2) cha Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa sura ya 200 Mapitio ya Mwaka 2022.

Hukumu dhidi ya Assan Jacob Kalinga imetolewa katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 10/2023, Novemba 18, 2024 Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mheshimiwa A. Lugome.

Kesi hiyo imeendeshwa na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Bi.Simona Mapunda.

Imeelezwa kuwa,mshtakiwa alifikishwa mahakamani baada ya kufanya ubadhirifu wa fedha kiasi cha shilingi 7,721,000 mali ya wanakijiji cha Mbuyuni walizochanga kulipia mita za Umeme wa REA kati ya mwezi Aprili, 2020 hadi Oktoba,2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news