Mwanasheria Mkuu wa Serikali atoa rai kwa Uongozi wa TLS

DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari amekutana na uongozi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na kuhimiza ushirikiano katika kuwatumikia Watanzania.
Akizungumza katika kikao kilichowakutanisha Uongozi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari amesema kuwa, TLS ni mdau muhimu katika kuishauri Serikali.
Ni kwa kubaini mambo muhimu yaliyopo katika utekelezaji wa sheria mbalimbali nchini na hivyo ujio huo ni hatua muhimu katika kuimarisha mahusiano baina ya pande hizo mbili.

Mwanasheria Mkuu ameyasema hayo Leo tarehe 1 Novemba, 2024 ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma wakati alipofanya mazungumzo na Uongozi wa TLS walipofika kwa ajili ya kujitambulisha, kufahamiana na kuboresha mahusiano baina ya ofisi hizo.
"TLS ni mdau wetu mkubwa hivyo tunathamini sana ujio wenu na tunaamini itaongeza wigo wa ushirikiano katika utendaji kazi,"amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rais wa TLS, Wakili Boniphace Anyisile Kajunjumele Mwabukusi amesema TLS inaiona Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni nyumbani hivyo pande hizi mbili zinapaswa kushirikiana kwa maslahi ya Wanasheria na Taifa.
"Tunapenda TLS ifanye kazi kwa maadili Uwakili wetu uwe credible tunaweza kushindana na kuvutia watu wa au aina tofauti tofauti kwa kuzungumza na kuimarisha Sheria kwa manufaa ya Taifa letu,"amesema Rais wa TLS.

Kwa upande wake Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno amesema, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sasa imepiga hatua kubwa katika matumizi ya mifumo mbalimbali ili kuimarisha na kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na mfumo wa OAG-MIS unaowezesha upatikanaji wa Sheria mbalimbali pamoja na sheria zote zilizofanyiwa marekebisho.
Aidha, Naibu Mwanasheria Mkuu amemuomba Rais wa TLS kutumia majukwaa yao kutangaza mafanikio ya mfumo huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news