DAR-Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha), Bi. Sauda Kassim Msemo, amekutana na ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Ushirikiano wa Maendeleo, Mhe. Balozi Ole Thonke. Kikao hicho hicho kimefanyika leo, tarehe 5 Novemba 2024, katika ofisi za makao makuu ndogo ya Benki Kuu jijini Dar es Salaam.