NAIBU WAZIRI SANGU AMPIGIA CHAPUO RAIS SAMIA, AWATAKA WANANCHI KUICHAGUA CCM JIMBONI KWELA

RUKWA-Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa wa Chama Cha Mapinduzi.
Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo leo kwa nyakati tofauti wakati akifanya Mikutano ya Kimkakati ya kumuunga mkono Rais Mhe.Samia Suluhu Hasan ya kuwachagua Viongozi katika Kata ya Mfinga, Kalumbaleza, Mwadui na Muze zilizopo katika Jimbo la Kwela mkoani Rukwa.

Amesema CCM ina kila sababu ya kushinda kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa jinsi ilivyojimbanua kushughulikia kero zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo.
Amesema wananchi wa Jimbo hilo wana kila sababu ya kuwapigia kura viongozi wa Serikali za Mitaa waliogombea kupitia chama hicho ikiwa ni ishara ya shukrani kutokana na mabilioni ya fedha ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anayoyatoa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.

"Tumejiandaa vilivyo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuhakikisha tunashinda kwa kishindo,"amesisitiza Mhe.Sangu.
Amesema katika kipindi chake cha Uongozi Mkoa wa Rukwa hususan Jimbo la Kwela limefunguka ambapo kila kona barabara zimeboreshwa huku zingine zikiendelea kuwekwa lami ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.

Amesema, huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, umeme pamoja maji zimeimarika ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Diwani wa Muze, Mhe.Kalolo Ntalli amesema kwa jinsi walivyojipanga na kutokana na ubora wa wagombea waliopitishwa na Chama hicho, hakika ushindi ifikapo tarehe 27 Novemba mwaka huu hauepukiki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news