Naibu Waziri Sangu apiga kura kijijini kwake mkoani Rukwa

RUKWA-Naibu Waziri, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ma Utawala Bora Mhe.Deus Sangu amesisitiza umuhimu wa Wananchi wa Jimbo la Kwela kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku akibainisha kuwa uchaguzi huu ni fursa kwa wananchi kupata viongozi wa karibu wanaojua changamoto zinazowakabili za moja kwa moja katika maeneo yao.
Mhe.Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Kwela ametoa kauli hiyo mapema leo Jumatano Novemba 27, 2024 mara baada ya kumaliza kupiga kura katika Kitongoji cha Pokopoko Kata ya Laela Mkoani Rukwa.
Akiwa ameonesha kuridhika na idadi ya wapiga kura waliojitokeza katika kitongoji hicho na jinsi mchakato wa uchaguzi unavyoendelea, Mhe.Sangu amewataka Wananchi waliobaki kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kupiga kura.
Amesisitiza kuwa ushiriki wa kila raia ni muhimu katika kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanikiwa kwa haki na uwazi, huku akiwapongeza wale ambao tayari wamepiga kura kwa kuwa mfano mzuri wa uzalendo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news