NAIBU WAZIRI UMMY AWASHUKURU RED CROSS NA TPA KWA MISAADA YA VIFAA SAIDIZI MAAFA YA KARIAKOO

DAR-Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy Nderiananga amewashukuru wadau kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross Tanzania) pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA kwa kutoa misaada ya vifaa saidizi kwa ajili ya kuendelea kusaidia katika zoezi la uokoaji linaloendelea kufuatia janga la kuporomoka jengo la ghorofa eneo la Congo na Mchikichi Kariakoo Wilaya ya Ilala kijini Dar es Salaam.
Ametoa shukrani hizo hii leo Novemba 19, 2024 na kueleza kuwa miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na machela tisa (9) mashuka 100 kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross Tanzania) Pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA, reflectors pamoja na cover white.
Naibu Waziri huyo ameendelea kutoa rai kwa wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kuchangia huku akipongeza namna zoezi la uokoaji linavyoendelea kwa kushirikiana na wadau.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news