Novemba 27 si mapumziko Zanzibar

ZANZIBAR-Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kuwa, hakutokuwa na mapumziko visiwani Zanzibar Novemba 27,2024 ambayo ni siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara,hivyo kazi zitatakiwa kuendelea kama kawaida.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar ambaye pia ni Msemaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hillary.

“Novemba 27 mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ameshatangaza kwamba siku hiyo itakuwa siku ya mapumziko kuruhusu wananchi wa Tanzania Bara kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kuchagua viongozi wao wa Serikali za Mitaa.

“Kwa vile Zanzibar hakuna uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawaarifu wananchi wote Jumatano Novemba 27,2024 ni siku ya kazi kama kawaida Zanzibar, ahsanteni.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news