DAR-"Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru.
"Nasi tunaungana na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa pole kwa familia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji),Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo, watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.
"Sisi Ofisi ya Msajili wa Hazina tutamkumbuka Bw. Mafuru kwa bidii, ubunifu unyenyekevu wake alipokuwa Msajili wa Hazina kuanzia Novemba 05, 2014 mpaka Desemba 07, 2016
"Mwenyezi Mungu aijalie familia umvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ampatie marehemu pumziko la amani;