DODOMA-Jeshi la Polisi Tanzania limesema hatua za uchunguzi wa matukio mawili makubwa yaliyojiri hivi karibuni likiwemo tukio la kushambuliwa kwa Deogratius Tarimo Novemba 11, 2024 katika eneo la Kiluvya,Pwani pamoja na tukio la kuporomoka kwa jengo la ghorofa huko Kariakoo Novemba 16, 2024 unaendelea.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime (DCP), amesema kuwa uchunguzi wa matukio hayo unaendelea vizuri na hatua za mwisho zinakaribia kukamilika.
“Upelelezi wa kesi hizi mbili upo katika hatua nzuri, na hivi karibuni taarifa kamili itatolewa kwa umma,” amesema DCP Misime.
Jeshi hilo limewahakikishia wananchi kuwa litatoa taarifa sahihi mara uchunguzi wa kina utakapokamilika.