IRINGA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limeanza uchunguzi ili kuwabaini watu wasiojulikana wanaodaiwa kumvamia aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Christina Kibiki na kumuua kwa kumpiga risasi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 13,2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,SACP ndc Allan Bukumbi;