DOHA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na ujumbe wake amewasili Doha, Qatar tarehe 3 Novemba 2024 na kuelekea Soko la Kihistoria la Souq Waqif.
Soko hilo la kihistoria ni moja ya kivutio cha utalii nchini humo ambapo huuza mavazi ya kitamaduni, viungo, kazi za mikono na zawadi.
Ziara hiyo fupi imeratibiwa na Naibu Mkuu wa Itifaki wa Qatar, Youssef Al Harami, kwa niaba ya Amiri wa Taifa la Qatar, Sheikh Tamim Bin Hamad Al Thani.