Rais Dkt.Mwinyi ahimiza amani na mshikamano

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindizi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameitahadharisha na kusisitiza jamii kuitunza amani na mshikamano hasa wakati wa uchaguzi unapokaribia nchini na kuiasa jamii kutotofautiana na kufarakiana wakati wa uchaguzi mkuu unapofika nchini na kuwataka kuendelea kuwa kitu kimoja.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo katika Masjid Hudaa, Machomane Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini, Pemba alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu kwenye Ibada ya sala ya Ijumaa.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema, Zanzibar inahitaji idumu kwenye amani huku akisisitiza kuwa maendeleo yoyote yana njia ya kufanikiwa kutokana na kuwepo kwa amani, umoja na utulivu na kusisitiza kuwa bila ya nchi kuwa na rasilimali ya amani hakutokuwa na jambo lolote litakalofanyika na kufanikiwa.
Kwa upande mwengine Alhaj Dk. Mwinyi pia amehudhuria dua maalumu ya kuiombea nchi kuendelea kuwa katika hali ya amani, umoja na utulivu ambayo imeandaliwa na Ofisi ya Mufti Zanzibar, imefanyika Masjid Rahman, Gombani Mpya, Mkoa wa Kusini Pemba.

Dua hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi pamoja na Wananchi wa mikoa yote ya Kusini na Kaskazini, Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news