ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amepongeza uamuzi wa Benki ya Stanbinc Tanzania wa kuwa na Tawi Zanzibar kwani kutaongeza idadi ya Benki na kurahisisha huduma kwa wananchi.

Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa ukuaji wa kasi wa Uchumi unaoendelea hivi sasa unahitaji kuwepo na mchango wa taasisi makini za kifedha.
Naye Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo Patrick Rutabanzikwa ameeleza kuwa maendeleo yanayoonekana Zanzibar hivi sasa na ongezeko la mahitaji ya taasisi za kibenki kwa wananchi kumechochea kwa Stanbic kufungua Tawi lake.