Rais Dkt.Mwinyi amefikisha maendeleo kila kona Zanzibar-Mheshimiwa Abdulla

ZANZIBAR-Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema, Wanachama wa CCM na Wazanzibari kwa ujumla wana kila sababu ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussen Ali Mwinyi kwa mafanikio na maendeleo makubwa aliyoiletea Zanzibar.
Ameyasema hayo katika Hafla Maalum ya Usiku wa Kumpongeza, Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi kwa kutimiza Miaka Minne ya mafanikio katika uongozi wake iliyofanyika katika Kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirizi Chake Chake Pemba iliyoandaliwa na Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar.

Amesema, katika Uongozi wa Rais Dkt. Mwinyi maendeleo ya wazi yanaonekana kila kona na hakuna eneo ambalo Dkt. Mwinyi hajalifikia kimaendeleo ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais ambae pia ni Mjume wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa amewataka Wazanzibari kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt.Mwinyi pamoja na Serikali anayoiongoza ili kumpa nguvu zaidi ya kuendelea kuwatumikia Wazanzibari kwa mafanikio makubwa zaidi.
Aidha, Mhe. Hemed amesema Rais Dkt.Mwinyi ni msikivu na mwenye kupenda umoja na mshikamano kwa wanachi wake hivyo Serikali anayoiongoza ipo tayari kupokea ushauri wenye tija utakaoileta Zanzibar maendeleo kwa maslahi mapana ya wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Sambamba na hayo amesema,mwaka wa tano wa uongozi wa Dkt.Mwinyi utekelezaji wake wa maendeleo utakuwa wa kupigiwa mfano ambapo miradi mingi na mikubwa ya maendeleo itakatekelezwa kwa lengo la kuendelea kunyanyua uchumi wa wazanzibari.

Naye Katibu wa Idara ya Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya CCM Zanzibar,Komredi Khamis Mbeto amesema, Chama Cha Mapinduzi kina kila sababu ya kumpongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa mema na mazuri anayoendelea kuwafanyia wananchi wa Zanzibar.
Komredi Mbeto amesema, wana CCM na wananchi wa Zanzibar wataendelea kumuunga mkono Dkt. Mwinyi kwa dhamira yake njema ya kuwaletea maendeleo Wazanzibari wote pasipo kujali rangi, kabila, dini wala jinsia zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news