Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mkewe Mama Mariam Mwinyi akisalimia na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdalla na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo Novemba 21,2024 akitokea nchini Zimbabwe kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA),Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliyofanyika Novemba 20,2024 jijini Harare, Zimbabwe.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mkewe Mama Mariam Mwinyi akisalimia na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea nchini Zimbabwe kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC.