ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Mhe.Iddi Said Khamis kuwa Kadhi wa Mahakama ya Kadhi ya Rufaa na ndugu Hiji Dadi Shajak kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji.
Hafla hiyo ya uapisho uliofanyika Ikulu Zanzibar tarehe 14 Novemba 2024 umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe.Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Hemed Suleiman Abdullla , Mawaziri, viongozi wa Dini na Vyama vya siasa.