Rais Dkt.Mwinyi awaapisha wakuu wa mikoa na wilaya aliowateua

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya aliowateua hivi karibuni.
Hafla hiyo ya uapisho imefanyika leo Novemba 23,2024 katika Viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja jijini Zanzibar.
Walioapishwa ni Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba,Mattar Zahor Masoud kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Sadifa Juma khamis kuwa Mkuu wa Wilaya ya Maghàribi A,Rashid Simai Msaraka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Abdalla Rashid Ali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba,Khatibu Juma Mjaja kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba.

Hamad Omar Bakari, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba,Mgeni Khatibu Yahya, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Pemba.

Othman Ali Maulid, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja,Cassian Gallos Nyimbo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati.

Juma Sururu Juma kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja na Hawah Ibrahim Bae kuwa Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zena Ahmed Said.

Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Mohd Said Dimwa, Viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa Dini na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news