Rais Dkt.Mwinyi ziarani China kushiriki Maonesho ya Saba ya China International Import Expo (CIIE)

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na ujumbe wake kuelekea Shanghai nchini China kushiriki katika Maonesho ya Saba ya China International Import Expo (CIIE), yatakayofanyika kuanzia Novemba 5 hadi 10, 2024.
Maonesho hayo yenye kaulimbiu “Enzi Mpya, Mustakabali wa Pamoja,” yanajumuisha Maonesho ya Biashara na Kongamano la Uchumi la Kimataifa la Hongqiao.

Tanzania imepewa heshima maalum kuwakilisha Bara la Afrika kutokana na mchango mkubwa wa zaidi ya kampuni 17 pamoja na sekta za kilimo, kazi za sanaa za mikono, bidhaa za kilimo na uchumi wa buluu.

Ushiriki wa Rais Dkt.Mwinyi katika maonesho hayo unatokana na mwaliko rasmi kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania.

Kabla ya kuelekea Shanghai nchini China, Rais Dkt. Mwinyi na ujumbe wake anatarajiwa kuwasili Doha nchini Qatar, ambapo atapokelewa na Naibu Mkuu wa Itifaki wa Qatar, Youssef Al Harami kwa niaba ya Amiri wa Taifa la Qatar, Sheikh Tamim Bin Hamad Al Thani, na kutembelea soko la kihistoria la Souq Waqif.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news