Rais Dkt.Samia aelekea nchini Brazil

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Novemba 16,2024 ameondoka nchini kuelekea Rio de Janeiro nchini Brazil kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa kundi la G20.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tarehe 16 Novemba, 2024 kabla ya kuelekea Rio de Janeiro nchini Brazil kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa kundi la G20. Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Brazil Mhe. Luiz Ińacio Lula da Silva ambapo pamoja na mambo mengine, atashiriki mijadala inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa na umasikini, kuchochea maendeleo endekevu na matumizi ya nishati mbadala.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news