Rais Dkt.Samia atoa shilingi bilioni 8 ujenzi na ukarabati viwanja vya mazoezi michuano ya CHAN 2025 na AFCON 2027

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi bilioni nane kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya mazoezi vitavyotumia kwa michuano ya CHAN 2025 na AFCON 2027.
Hayo yamebainishwa Novemba Mosi, 2024 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa wakati akisaini Mkataba wa ujenzi na Suma JKT katika ukumbi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa, fedha hizo zimetolewa za kuanzia ili kukamilisha kwa wakati kwa muda wa ndani ya siku 120 (miezi mitatu).
"Tayari mchakato umeanza wa ukarabati wa viwanja kikiwamo cha Meja Jenerali Isamuhyo, Gymkhana, Shule ya Sheria (Law School) na ujenzi wa viwanja vipya Leaders, Farasi, Tirdo na Gymkhana,"alisema Msigwa.
Alisema kuwa ujenzi huo utahusisha uwekaji wa taa, majukwaa yatayochukua watu 2000 katika viwanja vipya, njia za kupitisha maji na kupanda nyasi halisi ili kuendana na viwango vya CAF.Sambamba na CHAN na AFCON Serikali imekusudia kuwania kuwa wenyeji wa michuano ya "All African Games 2027".

Aliongeza kuwa Serikali ina mipango ni kujenga viwanja vitano vya mazoezi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Arusha.
Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya Suma JKT,Morgan Nyonyi alisema,wapo tayari kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
"Tayari kazi imeanza na leo hii tumesaini mkataba tu, tumeanza na Uwanja Meja Jenerali Isamuhyo ambapo, CAF walipita na kutupa baadhi ya maelekezo, na sasa tunaendelea na mchakato mzima wa uboreajaji na ujenzi wa viwanja vitano vya mazoezi," alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news