DAR-Novemba 20,2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewajulia hali na kuwapa pole majeruhi wa ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo ambao wamelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Ilala jijini Dar es Salaam.