ARUSHA-Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt.William Ruto ametangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Rais wa Jamhuri Sudan, Salva Kiir Mayardit ambaye amemaliza muda wake.
EAC inaundwa na nchi wanachama nane ikiwemo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamhuri ya Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Sudan ya Kusini na Somalia.
Dkt.Ruto ametangazwa leo Novemba 30,2024 katika Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.