DAR-Mkurugenzi Mkuu Mteule wa Shirika la Afya Dunia (WHO) Kanda ya Afrika, ambaye pia ni Mbunge wa Kigamboni,Dkt. Faustine Ndugulile ambaye amefariki usiku wa kuamkia Novemba 27,2024 nchini India anatarajiwa kuzikwa Jumatatu ya Desemba 2,2024 Kigamboni jijini Dar es salaam baada ya mwili wake kuagwa viwanja vya Karimjee.