Serikali inavithamini sana vyombo vya habari-Waziri Mchengerwa

DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amesema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inathamini mchango wa vyombo vya habari nchini kwani vina mchango chanya katika kuharakisha maendeleo katika sekta mbalimbali.
Mheshimwa Mchengerwa ameyasema hayo leo Novemba 12, 2024 jijini Dar es Salaam katika semina na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Semina hiyo ambayo imeandaliwa na OR-TAMISEMI ilikuwa mahususi kuangazia kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini.
“Kwa sababu ninyi ni watu muhimu sana kwa Taifa letu,mafanikio ya Taifa letu kupiga hatua ni kwa sababu ya kazi kubwa na kazi nzuri ambayo ninyi wahariri, waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mnafanya kwa Taifa letu.”

Waziri Mchengerwa amesema, mchango wa wadau hao wa habari nchini unatambuliwa katika nyakati zote toka Taifa lipate uhuru.
“Ndiyo sababu, msingi wa mambo yetu haya, msingi wa vyombo vyetu vya habari umeainishwa kwenye Katiba, umeainishwa kwenye sheria mbalimbali, kwenye miongozo na kwenye taratibu mbalimbali.

“Kwa hiyo nitambue kazi kubwa na nzuri ambayo mmeendelea kuifanya.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news