Serikali itaendelea kukabiliana na maradhi yasioambukiza-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema maradhi yasioambukiza ni tatizo linalokuwa na linalohitaji ushirikiano wa taasisi za ndani ya nchi na kimataifa katika kulipatia njia bora za kukabiliana nalo.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na timu ya Madaktari bingwa na Wataalamu wa Maradhi yasioambukiza kutoka Geneva waliofika Ikulu kuonana na naye tarehe 12 Novemba 2024.

Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa Zanzibar kama zilivo nchi nyengine duniani imekuwa na wagonjwa wa wengi wa Maradhi yasioambukiza wanaoongezeka kila mwaka hivyo inahitaji kuungwa mkono katika juhudi zake za kudhibiti ongezeko la wagonjwa wa aina hiyo.
Rais Dkt.Mwinyi amebainisha kuwa Zanzibar inabeba mzigo mkubwa wa Usafirishaji wa Wagonjwa kwenda nje ya nchi kutibiwa magonjwa mbalimbali ikwemo saratani hivyo suala la kujengewa uwezo Wafanyakazi wa sekta ya afya ni la umuhimu mkubwa.

Halikadhalika,Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kwa Wizara ya afya kuendelea na mchakato wa mazungumzo na timu hiyo ya Madaktari bingwa kwa dhamira ya kutafuta njia Bora utaalamu na upatikanaji wa dawa za kutibu Maradhi yasioambukiza.
Rais Dkt.Mwinyi amewahakikishia Madaktari bingwa hao kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana nao na kufanya kazi bega kwa bega kufanikisha lengo Lao la kuja nchini kubaini changamoto na maeneo ya Ushirikiano katika sekta ya afya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news