Serikali yaahidi maboresho zaidi kwa shule kongwe nchini

DODOMA-Serikali imeendelea kutenga fedha za ukarabati wa shule chakavu nchini zikiwemo shule za msingi katika Vijiji vya Kalundi, Lyapinda na Londokazi kadri ya upatikanaji wa fedha.
Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anyeshughulikia Elimu, Mhe. Zainab Katimba wakati akijibu swali la Mhe. Vicent Mbogo ,mbunge wa jimbo la Nkasi Kusini aliyetaka kujua mpango wa serikali kuhusu ukarabati wa Shule za Msingi katika Vijiji vya Kalundi, Lyapinda na Londokazi vilivyopo katika jimbo hilo.

Akijibu swali hilo Mhe. Katimba amsema “kuanzia mwaka 2022/23 hadi 2023/24, Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya ukarabati, ambapo shilingi bilioni 70.39 zimetolewa kwa ajili ya ukarabati wa shule 793 zikiwemo Shule za Msingi Chalantai, Nkundi na Sintali za Jimbo la Nkasi Kusini,” amesema.

Aidha, Mhe. Katimba amesema serikali katika mwaka wa fedha 2024/25 imetenga fedha kwaajili ya ukarabati wa shule kongwe na chakavu hatua inayoendelea ni kutathimini na itakapokamilika serikali itaweka kipaumbele kwenye shule yenye miundombinu chakavu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news