Serikali yaipongeza Taasisi ya Haydom kwa kutoa huduma bora za afya

MANYARA-Serikali imepongeza Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za Afya Haydom kwa utoaji huduma za afya ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuwapatia huduma bora za afya wananchi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geophrey Pinda akisisitiza jambo wakati akikakgua huduma za afya zinazotolewa na Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom tarehe 17 Novemba 2024 mkoani Manyara.

Hayo yamesemwa Novemba 17,2024 mbele ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mbulu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi,Mhe. Geophrey Mizengo Pinda (Mb.) akimwakilisha Waziri wa Fedha,Mhe.Dkt Mwigulu Nchemba kwenye Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya taasisi hiyo iliyopo wilayani Mbulu mkoani Manyara.

"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imatambua mchango wa kanisa katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwapatia wananchi huduma bora,"amesema Mhe.Pinda.
Sehemu ya waumini wa Kanisa la KKKT wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda (hayuko pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom yaliyofanyika Wilayani Mbulu mkoani Manyara tarehe 17 Novemba, 2024.

Mhe. Pinda amewaasa wanafunzi wa taasisi hiyo kutumia vema elimu wanayoipokea kwa kuendelea kujifunza kwa moyo wa kujitoa ili kuongeza ubunifu na kuondoa changamoto zinazoikabili sekta ya afya hapa nchini.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati wa Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom iliyopo wilayani Mbulu mkoani Manyara tarehe 17 Novemba, 2024.

"Nawaasa wanafunzi na wahitimu wa taasisi hii kuendelea kuwa na ari ya kujifunza, ubunifu na kujitolea katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya,"amesema Mhe. Pinda.

Naye Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Mbulu,John Nade ameishukuru Serikali ya Awamu wa Sita kwa kuiongezea taasisi hiyo nafasi za udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa Masomo 2024/25 na 2025/26.

"Tunaishukuru sana Serikali ya Jamhuri Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa uamuzi wake wa kuipa taasisi hii wanafunzi 60 kwa mwako 24/25 na wanafunzi 40 kwa mwaka 2025/26 kwa fani ya radiolojia,"amesema John Nade Msaidizi wa Askofu.
Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Fratei Gregory Massay akitoa shukurani zake wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom yaliyofanyika wilayani Mbulu mkoani Manyara tarehe 17 Novemba 2024.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini,Mhe.Fratei Gregory Massay amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kupeleka watumishi wa kutoa huduma katika taasisi hiyo.

"Niishukuru Serikali hasa Rais wetu wa Tanzania Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatusaidia watumishi watano mpaka sasa na sio hapa tu,hata hosptali yetu pia ametuletea,"amesema Mhe. Fratei Mbunge wa Jimbo Mbulu Vijijini.
Sehemu ya waumini wa Kanisa la KKKT wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda (hayuko pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom yaliyofanyika wilayani Mbulu mkoani Manyara tarehe 17 Novemba, 2024.

Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za Afya Haydom ilianzishwa kwa lengo la kusaidia kujenga uwezo wa kitaaluma na kutoa mafunzo bora katika nyanja mbalimbali za sayansi za afya na kuchangia kuboresha huduma za afya ndani na nje ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news