Serikali yawaondoa hofu wafanyabiashara Kariakoo kuhusu mali zao, biashara zaruhusiwa kuendelea isipokuwa maeneo haya

DAR-Serikali imewataka wafanyabiashara ambao walikuwa katika jengo la ghorofa lililoporomoka katika Mtaa wa Mchikichini na Manyema Kata ya Kariakoo jijini Dar es Salaam kuwa na subira, kwani imezihifadhi bidhaa zilizookolewa kwenye maghala salama na ziko chini ya usimamizi mzuri.
“Lengo tulikubaliana na wafanyabiashara tuzike kwanza, tuokoe ndugu zetu halafu ndiyo tuje kwenye suala la mali.

"Lakini pia, ilikuwa ni ngumu kuanza kuambiana mali hii ya nani, hivyo tukakubaliana zikusanywe sehemu moja na baada ya hii shughuli zoezi linalofuata ni kwenda kuangalia kila aliyekuwa na mali na imetoka humu ndani anaipata kihalali;

Hayo yamebainishwa leo Novemba 26,2024 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba wakati akizungumza katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Msemaji Mkuu wa Serikali, Makoba ametangaza kufunguliwa kwa maeneo yaliyokuwa yamefungwa ili biashara ziendelee tena.

“Tangu tarehe 16 sehemu nyingi za biashara zilifungwa na sababu nyingi ni usalama wa maisha na mali za watu.

"Sasa kwa leo tulipofikia,Serikali inatangaza kuwa maeneo yote ya Kariakoo yanafunguliwa kuendelea na biashara isipokuwa Mtaa wa Mchikichini unaokutana na Kongo, na kipande cha Mchikichini na Manyema.

“Eneo hili halitatumika kwa sababu kuna taratibu za kiuchunguzi zinaendelea,bado kuna majengo mawili yaliyo karibu na jengo lililoanguka kuna wataalam waje wajiridhishe kwamba yana usalama kiasi gani na taratibu zingine za kiuchunguzi."

Makoba ameeleza kwamba, baada ya taratibu hizo kukamilika wataalamu watashauri siku ambayo barabara itatumika kama awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news