MWANZA-Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imetembelewa na Mkurugenzi wa Mipango na mikakati kutoka Chuo cha Afya ya Jamii Columbia (Columbia University school of Public Health), Bi.Amy Gustavsson kutoka nchini Marekani lengo likiwa ni kutathmini huduma za matibabu katika maabara ya Usugu wa vimelea dhidi ya dawa za virusi vya UKIMWI, vina saba pamoja na Idara ya Huduma za Tiba na Matunzo (CTC).
Akizungungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Bahati Wajanga ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Tiba amewakaribisha na kuwapongeza kwa ushirikiano endelevu katika utoaji wa huduma za Maabara na CTC.
"Sisi kama Hospitali Tutaendelea kuunga mkono na kusimamia kwa uadilifu shughuli zote zilizo chini ya mashirikiano haya,"amesema Dkt.Bahati.
Aidha,Bi. Amy Gustovsson ameshukuru na kupongeza kazi nzuri inayoendelea kutolewa na kusimamiwa na Hospitali ya Bugando na kusisitiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo na madhumuni ya ushirikiano huu.