DAR- Klabu ya Simba imetangaza kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Francois Regis ambaye alikuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa klabu.
Pia,Bodi ya Simba imefanya uteuzi wa Zubeda Hassan Sakuru kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu.
Katika taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza kuwa, Zubeda yuko mbioni kuhitimu Shahada yake ya kwanza ya Uzamivu, ana Shahada mbili za Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza na Chuo Kikuu cha Mzumbe Tanzania. Pia ana Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Taarifa hiyo rasmi imeongeza kuwa,Zubeda amefanya kazi kama Meneja Miradi wa Simba akimsaidia Bw. Kajula kuhusu mchakato wa kutengeneza sera na ushauri wa masuala ya kiutendaji.