NA DIRAMAKINI
SIMBA Sports Club ya jijini Dar es Salaam imeanza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Bravos do Maquis ya Angola.
Mtanange huo umepigwa leo Novemba 27,2024 katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Bao la Jean Charles Ahoua kwa mkwaju wa penalti limeipatia Simba SC alama zote tatu huku golikipa Moussa Camara akiinusuru Simba SC kwa kuokoa mkwaju wa penalti.
Licha ya kupata ushindi mwembamba, Simba Sports Club ambayo inanolewa na Maahier Davids kwa sasa inaongoza Kundi A katika michuano hiyo kwa alama tatu.
Kundi hilo linaundwa na CS Sfaxien ya Tunisia ambao bado hawajacheza,Constantine ya Algeria ambao bado hawajacheza na Bravos do Maquis ya Angola ambayo ina alama sufuri baada ya mchezo wa leo.