Simba Sports Club yalaani vurugu kuelekea mchezo na Pamba Jiji FC

MWANZA-Uongozi wa klabu ya Simba umesikitishwa na vitendo visivyo vya kiungwana vilivyofanywa na viongozi wa timu ya Pamba Jiji FC, kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda kwa kutumia Askari Polisi mkoani humo.
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya NBC, Simba tulipaswa kutumia Uwanja wa CCM Kirumba kufanya mazozezi ya mwisho kuelekea mchezo wetu wa kesho Novemba 22, dhidi ya Pamba lakini hali isiyokuwa ya kawaida maafisa wa timu hiyo waligoma kutoka Uwanjani.

Pamoja na jitihada zote za kuwasihi, kupisha mazoezi lakini viongozi wa Pamba hawakukubali na kuendelea kusalia Uwanjani wakijifungia katika chumba cha mikutano.

Muda mfupi baadae mazoezi yakiwa yanaendelea, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa, Mtanda akiambatana na maafisa wa Polisi waliokuwa na vyeo mbalimbali huku wengine wakiwa na silaha walifika uwanjani hapo na kuingia ndani ya uwanja bila maelezo ya msingi wanakwenda kufanya nini.

Baada ya timu kumaliza mazoezi na kutaka kuondoka uwanjani, gari ya Polisi lilizuia msafara wa wachezaji na makocha huku wakiwakamata na kuwapandisha kwenye gari lao Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu na Kocha Msaidizi, Selemani Matola ambao waliwaachia baada ya mabishano.

Simba tunalaani matumizi ya nguvu yaliyotumika katika sakata hili na kuwakamata maafisa wa klabu yetu bila ya sababu za msingi kwani jambo hilo linaonekana kama jitihada za kudhoofisha timu yetu kuelekea mchezo wa kesho.

Baadae Rweyemamu na Matola waliachiwa na msafara kurejea hotelini.

Simba tunalaani vitendo vya matumizi ya dola katika mpira wa miguu, na tunawakumbusha viongozi wenye Mamlaka kutumia mamlaka yao katika njia sahihi.

Imetolewa na

Idara ya Habari na Mawasiliano

Simba Sports Club

21, Novemba 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news