Tanzania yafuzu AFCON 2025, yaichapa Guinea bao 1-0

DAR-Tanzania kupitia timu ya Taifa Stars ni miongoni mwa timu za Taifa zilizofuzu kushiri fainali za mataifa Afrika (AFCON) kwa mwaka 2025.
Ni baada ya leo Novemba 19,2024 katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuichapa Guinea bao 1-0.

Simon Msuva dakika ya 60' ndiye aliyerejesha heshima ya Taifa Stars kupitia bao pekee ambalo lilidumu kipindi chote.

Aidha, haya ni mafanikio muhimu kwa Taifa Stars chini ya Kocha Hemed Suleiman (Morocco).

Matokeo haya yanaiwezesha Tanzania kufuzu kwenda michuano ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON kwa mara ya nne.

Taifa Stars imeshashiriki michuano ya AFCON mara tatu 1980, mwaka 2019, mwaka 2023 na sasa inakwenda kushiriki kwa mara ya nne huko Morocco mwakani 2025.

Kwa sasa Kundi H waliopo kileleni ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa alama 12, Tanzania nafasi ya pili kwa alama 10,Guinea nafasi ya tatu kwa alama tisa huku Ethiopia ikiburuza mkia kwa alama moja.

Fainali zitachezwa nchini Morocco kuanzia Disemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news