RUVUMA-Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Ruvuma imeokoa fedha zaidi ya shilingi milioni 16,736,800 kwa kudhibiti vitendo vya rushwa na kuwafikisha mahakamani washtakiwa mbalimbali.
Miongoni mwa washtakiwa waliofikishwa mahakamani ni viongozi wa Majimaji Amcos Tunduru na Mzabuni aliyesambaza vifaa vya ujenzi Hospitali ya Wilaya ya Madaba ambapo washtakiwa walitiwa hatiani na Mahakama imewahukumu kulipa faini pamoja na vifungo
Hayo yamesemwa Novemba 18,2024 na Bi. Janeth Francis Haule ambaye ni Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma, wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa mkoa wake kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2024.
Tags
Habari
Programu Rafiki ya TAKUKURU
Ruvuma Region
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
TAKUKURU Tanzania