TANGA-Taasisi ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Tanga imeongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya shilingi Bilioni 1.9 yatokanayo na ada za Leseni za Biashara, Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni na Ushuru wa Huduma.
Hayo yamesemwa leo Novemba 9,2024 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga,Bw. Ramadhani Ndwatah wakati akiwasilisha Taarifa ya Utendaji Kazi ya Mkoa wa Tanga kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2024.
Hii imetokana na hatua zilizochukuliwa baada ya kubaini zaidi ya asilimia 64 ya wafanyabiashara kutokuwa na leseni za biashara na asilimia 90 kutolipa Ushuru wa Huduma na Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni jijini Tanga.
Pia umefanyika ufuatiliaji wa miradi 41 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 19.7