Tanzania yatajwa kinara kwa barabara bora barani Afrika

NA MWANDISHI WETU

TANZANIA imetajwa kuwa kati ya mataifa 10 bora barani Afrika ambayo yana miundombinu bora zaidi ya barabara.
Taarifa hizi zinakuja ikiwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kuanzia mijini hadi vijijini.

Uwekezaji huo unalenga kuwarahisishia wananchi, kufanya shughuli zao za kiuchumi ikiwemo usafirishaji kwa urahisi ili kuharakisha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mtandao wa Statista huku ikichapishwa na businessinsider, Tanzania katika 10 bora hizo ipo nafasi ya tisa ikiwa na alama 4.41.

             Nchi 10 Afrika zenye miundombinu bora ya barabara 2024 

Nafasi                           Nchi                      Alama              

1

Namibia

5.57

 

2

Misri

5.53

 

3

Benin

5

 

4

Rwanda

4.86

 

5

Mauritius

4.8

 

6

Ivory Coast

4.64

 

7

Morrocco

4.62

 

8

Kenya

4.42

 

9

Tanzania

4.41

 

10

Afrika Kusini

3.97

 

Chanzo:statica /businessinsider

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news