Tanzania yatoa uzoefu kwa Uganda namna bora ya kuendesha Sekta ya Madini

DAR-Ikiwa ni siku ya tatu ya Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Sekta ya Madini Tanzania leo Novemba 21, 2024 Wizara ya Madini Tanzania yatoa uzoefu kwa Chemba ya Migodi ya Uganda kuhusu mbinu bora za kuendeleza Sekta ya Madini.

Tanzania ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo, yatoa uzoefu kuhusu namna bora ya kusimamia wachimbaji wadogo wa madini, ukusanyaji wa mapato ya kodi, biashara ya madini, uongezaji thamani madini pamoja na njia bora za Uendelezaji endelevu wa sekta kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na taifa.
Akizungumza katika mkutano uliojumuhisha wataalam kutoka Chemba ya Migodi nchini Uganda na Chemba ya Migodi Tanzania, Naibu Katibu Katibu Msafiri Mbibo amesema kuwa, Tanzania ina uzoefu mkubwa katika Sekta ya Madini kwa kipindi kirefu imekuwa mshauri kwa mataifa mengine yanayohitaji kuboresha sekta hii ambayo kwa asilimia kubwa imekuwa inatoa mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa.
Akichangia kuhusu usimamizi wa wachimbaji wadogo , Kamishna msaidizi Francis Mihayo amesema kuwa , wachimbaji wadogo ni moja ya kipaumbele cha Wizara ya Madini kwa kuhakikisha sekta hii inachangia kikamilifu kwenye Pato la Taifa na kuleta maendeleo ya kiuchumi na jamii.

Mihayo ameeleza kuwa , Serikali inachukua hatua mbalimbali za kuwaendeleza wachimbaji wadogo ikiwa pamoja na kutoa elimu na mafunzo ya kitaalam katika uchimbaji, upatikanaji wa leseni, upatikanaji wa mahitaji na vifaa , uimarishaji wa masoko na uboreshaji wa miundombinu.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya madini , Mhandisi Ramadhani Lwamo amesema kwenye mnyororo wa thamani madini kuna aina mbalimbali za kodi ikiwemo kodi ya mapato, Kodi ya Mrabaha , Kodi ya Ada za Madini.
Mhandisi Lwamo ameongeza kuwa, pamoja na kodi hizo pia kuna maswala ya ukaguzi ambayo pia ni muhimu katika sekta hii akitaja aina za Ukaguzi kuwa ni pamoja na Ukaguzi wa uzalishaji wa madini na Ukaguzi wa madini yanayosafirishwa.

Naye, Katibu Mtendaji wa Chemba ya Migodi Tanzania Mhandisi Benjamini Mchwampaka amesema , mashauriano haya ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kubadilishana uzoefu kati ya nchi hizi mbili.

Pamoja na mambo mengine , Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi na Nishati ya Petroli , Ashaba Aggrey ameishukuru Tanzania kwa mawazo mazuri juu ya usimamizi wa sekta ya madini hususan katika hatua mbalimbali zinazounganisha sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi.
Mkutano huo umeudhuriwa na wataalam mbalimbali kutoka Chemba ya Migodi ya Tanzania na Uganda , Wizara ya Madini, Tume ya Madini na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news