TANZIA:Mwanamuziki Mzee King Kikii afariki

DAR-Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba mwanamuziki mkongwe, Boniface Kikumbi Mwanza Mpango (King Kikii) amefariki dunia.
King Kikii ambaye ameugua kwa muda mrefu, amefariki usiku wa kuamkia leo Novemba 15,2024 katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.

Mzee King Kikii atakumbukwa kwa wimbo wake uliotamba zaidi wa Kitambaa Cheupe.

Mzee Kikii alizaliwa Januari 1, 1947 katika mji wa Lubumbashi uliopo katika mkoa Katanga huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 

Aidha,alikuwa ni mtoto wa tano kwa kuzaliwa toka kwa wazazi wake mzee Katambo Wabando Paulino na mama yake Mwanza Jumban Elia Maria.

King Kikii aliingia hapa nchini kwa mara ya miaka ya 1970 alipofuatana na bendi ya Orchestra Fouvette toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakati huo ilikuwa ikitwa Zaire.

Baadaye, King Kikii alijijengea umaarufu kwa wapenzi wa muziki wa dansi, kila kona hapa nchini kwa kutoa burudani katika sherehe mbalimbali zikiwemo za Kitaifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news