TCDC kuimarisha ushirika wa mazao ya bustani mkoani Arusha

ARUSHA-Timu ya maafisa kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika ikiongozwa na Mrajis Msaidizi - Masoko na Uwekezaji, Revocatus Nyagilo imekutana na kufanya majadiliano na shirika la RIKOLTO, WORLD VEGETABLE CENTER pamoja na Chama Kikuu cha Ushirika Arusha (ACU).
Majadiliano hayo yamelenga katika kuimarisha Vyama vya Ushirika wa mazao ya bustani kupitia wadau kwa kuunganisha na Masoko ya mazao na bidhaa zinazozalishwa na Vyama vya Ushirika, uboreshaji wa miundombinu itakayowezesha ongezeko la thamani ya mazao ya wakulima, ujenzi wa maghala, ununuzi wa mizani za kidigitali na upatikanaji wa vitendea kazi vitakavyorahisisha utengamafu wa mifumo ya mawasiliano ya Vyama.

Majadiliano hayo yamefanyika leo Novemba 15, 2024 kwenye ofisi za wadau hao mkoani Arusha.

Masuala mbalimbali yamejadiliwa yakiwemo upatikanaji wa masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi, mitaji toshelevu, upatikanaji wa pembejeo na huduma za ugani, miundombinu ya umwagiliaji na usafirishaji wa mazao pamoja na utunzaji wa mazao.

Mrajis Msaidizi Nyagilo amebainisha kuwa majadiliano hayo ni miongoni mwa hatua za msingi katika uimarishaji wa Vyama vya Ushirika wa mazao ya bustani katika utekelezaji wa mradi ili kuwa na endelevu wa Vyama hivyo.

Aidha , ACU imeshauriwa kuweka kwenye mikakati yao kutoa huduma za ugani, pembejeo na Masoko ya AMCOS za mazao ya bustani zilizopo katika wilaya za Arusha, Karatu na Meru.

TCDC na wadau hao, wameazimia kuwepo kwa Randama ya Makubaliano (MoU) ili kuweza kubainisha maeneo ya kufanyia kazi.

Aidha, Nyagilo ameeleza kuwa kazi hiyo ya kukutana na wadau inatekelezwa katika Mikoa mitatu (3) ya Arusha, Dar Es Salaam na Iringa kati ya mikoa 12 ikiwa ni hatua ya awali na kuendelea kwa Mikoa mingine yenye wadau wengi wa mazao ya bustani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news