TCDC yakutana na wadau wa mnyororo wa thamani katika mazao ya mbogamboga

DAR-Timu ya maafisa kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika (Tanzania Cooperative Development Commission-TCDC) ikiongozwa na Mratibu wa mradi wa uhamasishaji na uanzishaji wa Vyama vya Ushirika Mrajis Msaidizi Ibrahim Kadudu imekutana na kufanya majadiliano na Mashirika ya Agriterra pamoja na USAID Farmer to Farmer Programme.
Majadiliano hayo ya Utekelezaji wa mradi wa uhamasishaji na uanzishaji wa vyama vya ushirika vya mazao ya mbogamboga na bustani yameendelea kwa lengo la kuendelea kuwaunganisha wadau wa mnyororo wa thamani wa mazao hayo na vyama vya ushirika katika ofisi za wadau Novemba 11,2024 jijini Dar es Salaam.

Masuala mbalimbali yamejadiliwa yakiwemo upatikanaji wa masoko, mitaji, pembejeo, miundo mbinu ya umwagiliajipamoja na utunzaji wa mazao.
Mrajis Msaidizi Kadudu amebainisha kuwa majadiliano hayo ni miongoni mwa hatua za msingi katika utekelezaji wa mradi kwa kuwa ndio hutoa uhakika wa muendelezo wa vyama hivyo baada ya kusajiliwa.

Aidha, Kadudu ameeleza kuwa kazi hiyo ya kukutana 9na wadau inatekelezwa kwa Mikoa ya Iringa, Arusha na Dar Es Salaam ikiwa ni hatua ya awali na kuendelea kwa Mikoa mingine yenye wadau wengi wa mazao ya mbogamboga na bustani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news