DAR-Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imekutana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na kujadiliana upatikanaji wa masoko kwa Vyama vya Ushirika vya mazao ya mbogamboga na bustani ndani na nje ya nchi Novemba 12, 2024 jijini Dar es Salaam.
Kupitia kikao hicho TCDC iliwakilishwa na ndugu Tumaini Chaulema na TANTRADE iliwakilishwa na ndugu Crispine Luanda na ndugu Petro Matulanya
Maazimio mbalimbali yalifikiwa ikiwemo kuweka mpango wa kuweka Makubaliano ya utendaji kazi wa pamoja ili kurahisisha fursa za wakulima wa mazao ya mbogamboga kupitia vyama vya ushirika vilivyosajiliwa.
Tags
Habari
Tanzania Cooperative Development Commission (TCDC)
TCDC Tanzania
Tume ya Maendeleo ya Ushirika