DAR-Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesisitiza kuwa, Muhamed Ame alikuwa ni miongoni mwa wachezaji 23 waliokuwa wameorodheshwa kwa ajili ya mechi dhidi ya Guinea.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF, kabla ya mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Novemba 19,2024 wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) walikaguliwa na timu pinzani pamoja na kamishna wa mchezo huo, kabla ya kuruhusiwa kucheza.
“TFF haina taarifa yoyote kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuwa ushiriki wa Ame katika mechi hiyo haukuwa halali,” ilisomeka taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa wa za TFF.