DAR-Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (Tanzania Football Federation-TFF) limetoa pole kwa wananchi na wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Ni kutokana na ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa nne katika Mtaa wa Congo na Mchikichi ndani ya Kata ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.
"Tunatoa pole kwa wote walioathirika kufuatia kuporomoka kwa jengo Kariakoo, Dar es Salaam, Mungu awalaze mahala pema wote waliopoteza maisha, pole Kariakoo,"imeeleza sehemu ya taarifa ya TFF kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Ajali hiyo imetokea Novemba 16,2024 ambapo jitihada za Serikali kwa kushirikiana na wananchi zinaendelea katika kufanya uokoaji.