DAR-Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Tigo Tanzania imebadilishwa jina na sasa itajulikana kama YAS kuanzia leo Novemba 26,2024.
Mabadiliko hayo yametangazwa leo katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali alikuwa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas,Jerome Albou amesema, sababu ya mabadiliko hayo inatokana na uwekezaji uliofanyika miaka miwili iliyopita.
"Tigo Zantel ilikuwa ni sehemu ya chapa, hivyo itaendelea kubaki hivyo. Sababu kubwa inayotufanya tubadilike ni kwa sababu miaka miwili iliyopita tulipata chapa mpya na Tigo na Zantel ziliunganika, hivyo ukiwa Bara na Visiwani kwa sasa jina ni moja, Yas."
Naye Afisa Mkuu Mixx by Yas,Angelica Pesha amesema kuwa, "Leo tumebadilika kama Tigo na Tigo Pesa. Leo sisi ni wapya tunaitwa Yas na Mixx. Yas ni kama Yes,lakini ni Yes yenye Excitement.
"Na tunasema Yas kwa sababu tunajua kuna mambo mengi sana tunajua yanakuja na tuko excited.
"Tulianza kama Mobitel, ikaja Buzz, ikaja Tigo na ni miaka mingi. Na tassisi sisi ni kama bianadamu tunabadilika.
"Miaka 30 nyuma haukuwa hivi, unakamilika kila siku na sisi tunabadilika kuwapa kitu kizuri sana na Tigo imefanya kazi nzuri sana kwa miaka 30."