DAR-Kikosi cha Timu ya Taifa cha Guinea kimewasili jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo Novemba 18, 2024.
Ujio wao nchini ni kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania.
Mtanange huo utapigwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Licha ya Guinea kuingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza 2-1 dhidi ya Taifa Stars kwenye mchezo wa kwanza,pia mchezo huu ni muhimu kwa Taifa Stars kwani ikipata ushindi itasonga mbele.