TMA yaeleza athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye kilimo cha mwani

BAKU-Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Zanzibar, Masoud Faki ameeleza namna kilimo cha mwani kinavyoweza kuathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi.
Ameyaeleza hayo leo Novemba 22,2024 wakati akiwasilisha mada katika Banda la Tanzania, lililopo kwenye Mkutano wa 29 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29), unaofanyika Baku,Azerbaijan.

Ameeleza kuwa,kilimo cha mwani kinaathiriwa zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa hususani mvua nyingi,joto kali na upepo mkali.

Aidha, amefafanua kuwa TMA inatoa huduma za utabiri ikiwemo Msimu na utabiri wa hali mbaya ya hewa wa siku tano ambao huwezesha wakulima kufanya maamuzi sahihi kama vile uchaguzi wa eneo linalofaa ili kukabiliana na hali ya mvua nyingi ambayo husababisha upungufu wa kiwango cha chumvi na hivyo kusababisha magonjwa.

Pia,maamuzi mengine ni uvunaji wa zao hilo ili kukabiliana na upepo mkali unaoweza kuleta madhara ya mwani kukatika na kupotelea baharini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news