NA GODFREY NNKO
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa katika maeneo machache ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi na kwingineko nchini.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 30,2024 na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuanzia Novemba 30,2024 hadi Desemba 2,2024 ambapo mamlaka imetoa angalizo.
Mvua hiyo inatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ukiwemo Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe na Rukwa.
Pia,kwa Ukanda wa Pwani ya Kusini mwa Bahari ya Hindi mvua hiyo inatarajiwa kunyesha mikoa ya Lindi na Mtwara.
Aidha, kwa Kanda ya Kati, mamlaka hiyo imebainisha mvua inatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dodoma na Singida na Kanda ya Kusini ni Mkoa wa Ruvuma na Morogoro.
Katika hatua nyingine, TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi ikiwa ni katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa na Songwe,
Ukanda wa Pwani ya Kusini mwa Bahari ya Hindi mikoa ya Lindi na Mtwara, Kanda ya Kati mikoa ya Dodoma na Singida na Kanda ya Kusini mkoa wa Ruvuma na Morogoro.
Tags
Habari
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Mikoa ya Tanzania
Mvua Kubwa
Tanzania Meteorological Agency (TMA)